Loading...

Thursday, 24 May 2018

Tuesday, 22 May 2018

Hii Ndio Adhabu na Faini Utakayo Pewa Utakapokutwa Umevaa Sare za Jeshi Bila Ruhusu..Faini Itakuacha Mdomo Wazi.

Hii Ndio Adhabu na Faini Utakayo Pewa Utakapokutwa Umevaa Sare za Jeshi Bila Ruhusu..Faini Itakuacha Mdomo Wazi.


#IjueSheria: Mtu yeyote ambaye hatumikii Jeshi la Ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala Jeshi lolote la Polisi lililowekwa kwa Sheria akivaa bila ruhusa ya Rais vazi rasmi la Jeshi lolote au vazi linalofanana na vazi rasmi au kuwa na alama yoyote ya Kiaskari atakuwa ametenda kosa

Mtu aliyetenda kosa hilo atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha mwezi mmoja jela au faini ya Tsh. Mia mbili

Aidha, hakuna kifungu kinachomzuia mtu yeyote kuvaa vazi rasmi katika michezo ya tamasha inayochezwa hadharani mahali popote iwapo ataliwakilisha Jeshi kwa nia njema 
Breaking News: Maafisa Watatu wa TIC Wafariki Dunia Kwenye Ajali ya Gari

Breaking News: Maafisa Watatu wa TIC Wafariki Dunia Kwenye Ajali ya Gari

Breaking News: Maafisa Watatu wa TIC Wafariki Dunia Kwenye Ajali ya Gari

MAOFISA watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini  (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika  ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.


Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).


Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus. Wote walikuwa wakielekea Dodoma kwa ajili ya mkutano ambao unatakiwa kufanyika leo Jumanne jijini humo.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.