Mlinga Aomba Radhi Watanzania Baada ya Kujigeuza Daktari Kumchoma Sindano Mwanafunzi.

4:51:00 PM

Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga amewaomba radhi Watanzania kwa tukio alilolifanya la 'kujigeuza daktari.'

Akizungumza na MCL Digital katika viwanja vya Bunge leo Mei 3, 2018, amesema aliitwa kuhudhuria uzinduzi wa chanjo na wala yeye si mtaalamu wa afya.

"Kitaalamu mimi ni mtawala si daktari, nilifanya nilivyoelekezwa na sikufahamu madhara yake wanasema kitabibu huruhusiwi kushika hata sindano," amesema Mlinga na kuongeza:

"Kuomba msamaha si woga, sisi tulioendelea nasema kunradhi."

 Mlinga amesema hayo baada ya picha yake kuzagaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha anamdunga sindano binti wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana jimboni mwake.

 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizungumzia suala hilo bungeni na kusema ingawa viongozi hao hawakuwachoma sindano lakini ni makosa kushika hata sindano. 

Related Posts

Previous
Next Post »